Waziri wa Afya Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ameagiza kuondolewa kwa Kiongozi anayesimamia Ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mwalimu Nyerere Mkoani Mara kutokana na kutoonekana kazini katika ziara zake tatu.
“Bahati mbaya nasikia ni mwanamke na muda mwingine sisi wanawake tukipewa majukumu makubwa tunaboronga naagiza asikanyage hapa hospitali kwani haturidhiki na utendaji kazi wake,” Waziri Ummy