Wote tunafahamu kwamba rapper 50 cent anajua kutumia fursa za kuweza kujitengenezea fedha. Lakini safari hii biashara zake zimemletea matatizo kupitia kesi iliyodumu kwa miaka 3 kati yake dhidi ya kampuni ya kutengeneza earphone – Bradenton.
Kwa mujibu wa mtandao wa www.hot97.com, ni kwamba 50 Cent ameamriwa na mahakama kuilipa kampuni hiyo kupitia kitengo chake Sleek Audio karibia $4.5 million kama fidia ya malipo mwanasheria na $11.7 million kama fidia ya kuvunjika kwa mkataba na kampuni hiyo ambayo ilikuwa wakishirikiana kutengeneza 50 Cent headphones.
50 Cent mwanzoni alituhumiwa kuiba designs za Sleek Audio, ambazo mwanzoni alipewa kwa ajili kuzipitisha kwa ajili ya kuanza kwa uzalishaji wa headphones hizo, lakini baadae 50 aliwageuka Sleek na akaamua kushirikiana na kampuni nyingine kutumia designs alizopewa na kampuni ya Sleek.