Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli, amesema kuwa katika kipindi chake cha uongozi wachimbaji wa wadogo wa madini wamekuwa wakipewa leseni pale wanapogundua maeneo yenye dhahabu badala ya kufukuzwa.
JPM amezungumza Geita nakusema kuwa tofauti na siku za nyuma wachimbaji wadogo wanahesabiwa kama wawekezaji nchini.
“Siku za nyuma ilikuwa ukishagundua dhahabu wanafukuzwa wanakuja wakubwa ukipata mahali unafukuzwa wanakuja wengine tukasema hapana! wakigundua wanabaki palepale na wanapewa leseni na wao waweze kutajilika kwasababu tunawahesabu wao kama wawekezaji” Rais Magufuli.
“Tumejitahidi kuwawezesha wachimbaji wadogo kwa kuwatengea maeneo, kufuta ama kupunguza viwango vya kodi walivyokuwa wanalipa na kuwapatia mafunzo na mitambo ya kuendesha shughuli zao za uchimbaji” Rais Magufuli