Mgombea urais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia chama cha ACT Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad ameonyesha wasiwasi wa kukwamishwa katika kuwania kinyang’anyiro hicho.
Akizungumza katika kongamano la vijana wa ACT Wazalendo, lililofanyika visiwani Zanzibar Maalim Seif amedai kuwepo kwa baadhi ya watu wa vyama vingine ambao wamepanga kumuwekea pingamizi katika Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), ili asiteuliwe kugombea.
“Nasikia kuna watu washapangwa na vyama vingine kuniwekea pingamizi, nawakaribisha kwa sababu kuniwekea pingamizi, atakuja kutoa hoja zake na ushahidi wake, na mimi naujua vilevile” Maalim Seif
” Sioni kama kuna pingamizi yoyote, kama itasimama juu yangu, mimi nimezaliwa Mtambwe hamjui ninyi? Ndiyo sifa ya kwanza ya mgombea urais, awe Mzanzibari wa kuzaliwa sio Mzanzibari mkaribishi” Maalim Seif
‘WAOMBE MSAMAHA WANANCHI WAKO” MAGUFULI AMTAKA MGOMBEA UBUNGE AOMBE MSAMAHA