Chama cha Wahasibu Tanzania (TAA) kupitia kwa Mwenyekiti wake Peter Lucas Mwambuja kimewatunuku vyeti wanafunzi wa kidato cha sita waliofanya vizuri katika masomo ya mchepuo wa Biashara.
Lengo Kuu la kufanya hivyo ikiwe ni sehemu ya kuendeleza na kuchochea ukuaji wa taalum ya uhasibu na masuala ya fedha Tanzania na kuendelea kuzalisha wanataaluma wapya.
Mwenyekiti wa TAA Peter Lucas alieleza kuwa wakati huu nchi ikiwa imeingia uchuni wa kati sekta ya uhasibu na usimamizi ni miongoni mwa sekta ambazo zimechangia pia hatua hiyi Tanzania iliyopiga.
”Sisi kama wanataaluma wa taaluma hii hadhimu tunatambua kwamba katika juhudu za taifa letu kupiga hatu mbele kwenye uchumi wa kati mchango wa taaluma ya uhasibu ni mkubwa sana”>>> Peter Lucas
Maamuzi hayo yaliofanyika ya kuwatunuku vyeti wanafunzi wa kidato cha sita wa kike na kiume waliofanya vizuri 2020 yalifanyika katika baraza la 18 la chama cha Wahasibu katika kikao cha tatu cha kawaida baada ya kuagiza uongozi wa chama hicho kuwasiliana na serikali na kuchangia kwa kutoa waalimu wa masomo hayo.