Tetesi za usajili wa mchezaji wa FC Bayern Munich Toni Kroos zimezidi kutengeneza vichwa vya habari katika media.
Wakati mapema wiki hii kocha wa Bayern Pep Guardiola akisema kwamba hatma ya mchezaji ipo mikononi mwake mwenyewe, leo hii wakala wake amezungumza na kauli inayoonyesha mchezaji huyo anaweza kubaki Bayern Munich mpaka mkataba wake utakapoisha mnamo 2015.
Muda mfupi baada ya Guardiola kusema kwamba hatma ya mchezaji ipo mikononi mwake mwenyewe, gazeti la Guardian la Uingereza likaripoti kwamba Manchester United imempa ofa ya mshahara wa paundi 260,000 kwa wiki, fedha ambayo itakuwa ni mara nne ya anayopata sasa 72,000 pounds kwa wiki.
Lakini leo Jumatano wakala wa mchezaji huyo Volker Struth, amesema United haijawafuata rasmi kuhusu suala la kutaka huduma za mchezaji huyo.
Alisema: “Hakuna ofa rasmi ya mkataba na Bayern. Pia zaidi sidhani kama kuna hitaji la kutoa ofa mpya, kwa sababu Toni Kroos ataendelea kuichezea Bayern mpaka 2015.”
Wakala huyo ameshaonekana akiwa pamoja na kocha United David Moyes takribani mara mbili katika miezi ya hivi karibuni.