Mahakama ya Jumuiya Afrika Mashariki imetupilia mbali madai ya kupinga uhalali wa Muungano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yaliyofunguliwa na baadhi ya wanaharakati.
Mapema leo Wakili Mkuu wa Serikali Gabriel Malata ameeleza kuwa mahakama hiyo imetoa uamuzi huo baada ya kukubaliana na hoja zote za upande wa Serikali ikiwa ni pamoja na madai kuletwa nje ya muda, pamoja na uhalali wa mahakama kuhoji uhalali wa muungano huo.
Amesema Mahakama ya Afrika Mashariki imezaliwa kupitia makubaliano (The East African Community Treaty) ya mwaka 1999 na kuanza kufanya kazi mwaka 200, hivyo mahakama hiyo haina mamlaka ya kuhoji Muungano wa Tanganyika na Zanzibar wa mwaka 1964.