Mtu wa kwanza kutibiwa Virusi vya UKIMWI Timothy Ray Brown amefariki kutokana na saratan, Brown ambaye pia alijulikana kama mgonjwa wa Berlin alipandikizwa bone marrow kutoka kwa mtu ambaye alikuwa na kinga dhidi ya HIV 2017.
Hii ilimaanisha kwamba alikuwa ahitaji tena dawa za kukabiliana na Virusi vya UKIMWI hivyo basi alibakia bila maambukizi yoyote ya virusi hivyo vinavyosababisha UKIMWI kwa maisha yake yote.
Shirika la kimataifa kuhusu wagonjwa wa ukimwi duniani limesema kwamba Brown aliupatia ulimwengu matumaini kwamba dawa ya kutibu UKIMWI inaweza kupatikana.