Marekani ikiwa katika kipindi cha uchaguzi habari kutoka Italia zinasema Vatican imemkatalia Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Mike Pompeo kuonana na Papa Francis.
Kiongozi huyo wa juu wa Kanisa Katoliki ameelezwa kuwa hawapokei wanasiasa wakati wa kipindi cha uchaguzi.
Hatua hiyo inaongeza hali ya mzozo wa kidiplomasia baada ya kauli ya Pompeo kuhusu China na Kanisa Katoliki, Vatican ilimshutumu Pompeo kuwa anajaribu kutumia suala hilo kuvutia wapiga kura wa uchaguzi wa urais wa mwezi Novemba nchini Marekani.
Katika makala ya mwanzoni mwa mwezi Septemba, Pompeo amesema Kanisa Katoliki linapoteza ”mamlaka yake ya kinidhamu” kwa kufanya makubaliano mapya na China kuhusu uteuzi wa Maaskofu.
MTU WA KWANZA KUPONA UKIMWI AFARIKI, ALIPANDIKIZWA UBOHO (BONE MARROW) ALITUMIA MAMILIONI KUPONA