Changamoto ya wakulima kutokopesheka na taasisi mbalimbali za fedha hapa nchini imepatiwa ufumbuzi baada ya benk ya CRDB kuanzisha akaunti ya FAHARI KILIMO ambapo wakulima wametakiwa kuchangamkia fursa ya mkopo huo maalum ambao utaboresha kilimo chao kuwa chenye tija.
Meneja wa benk ya CRDB kanda ya kaskazini Chiku Issa ametoa wito huo mjini Moshi katika tawi la Mbuyuni wakati wa uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja inayoadhimishwa duniani kote kila ifikapo mwezi Oktoba kila mwaka,ambapo benk hiyo imeandaa shughuli mbalimbali katika kipindi cha wiki mbili zitakazofanyika katika matawi yote ya benk hiyo.
Akizungumza katika hafla hiyo iliyoambatana na burudani kutoka kwa wafanyakazi wa CRDB wa matawi ya Mkoa wa Kilimanjaro na wateja Chiku amesema benki inaungana na taasisi nyingine duniani kuadhimisha siku hiyo kwa kuwahudumia wateja na kuwahamasiha kutumia fursa mbalimbali zinazotolewa na benk hiyo ili kuboresha maisha yao.
Amesema benk hiyo imekuja na bidhaa nyingi tofauti tofauti ambazo zinagusa jamii ya kila kada ambapo akiizungumzia akaunti ya kilimo amesisitiza kuwa akaunti hiyo haina makato ya aina yeyote na itawasaidia kuendeleza kilimo chao ambacho kimekuwa hakiendelei kwa miaka nenda rudi.
Chiku amesema CRDB imejipanga kuhakikisha kila wakati wanawafikia wateja wao wote huku wakisisitiza suala la ushirikiano na kujenga timu moja.
Amesema CRDB itaendelea kuboresha huduma zake ili kila mtanzania na kila mteja wa CRDB ziweze kumgusa na kuweza kupata mikopo kwa urahisi ili kuboresha maisha yao na kwenda na uchumi wa kati.
CRDB pia imekuwa na bidhaa mbalimbali kama akauti ya afya kwa watoa ambayo hutoa huduma ili kwa kuwanunulia vifaa wafanyabiashara wa sekta ya afya,CRDB pia wanatoa mikopo ya ujenzi wa miundombinu,ambapo benki hiyo pia haijawasahau wateja wadogowadogo almaarufu kama wamachinga ambao nao wana mikopo maalum kwa ajili yao.
Mikopo mingine inaytolewa na CRDB ni mikopo ya vikundi mikopo ambayo wateja hutumia vitambulisho vya wamachinga kujidhamini na kupata mkopo.