Mahakama kuu kanda ya tanga kwa kushirikiana na wadau wake,imeshuhudia zoezi la uteketezaji madawa ya kulevya ainaya Heroin gramu 351.99 kwenye shauri la uhujumu uchumi namba 4 la mwaka 2019 kati ya jamuhuri na mshatikiwa Mussa Sembe,baada ya hukumu kutolewa mwezi julai mwaka huu.
Uamuzi huo umefikiwa na mahakama hiyo baada ya kumkuta mshatikiwa hana hatia katika kesi iliyokuwa iliyokuwa ikisikilizwa na Jaji Lilian Mashaka wa Mahakama Kuu ya Tanzania, kitengo cha makosa ya rushwa na uhujumu uchumi.
Akizungumza na wanahabari mara baada ya kuteketeza madawa hayo katika kiwanda cha saruji Tanga cement, Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Tanga Francis Kabwe amesema mara baada ya hukumu kutolewa mahakama hiyo ili amuru madawa hayo kuteketezwa.