Rais wa Marekani Donald Trump amesema ataiondoa Sudan katika orodha ya wafadhili wa ugaidi iwapo italipa fidia ya dola Milioni 335 (£259m).
Waziri Mkuu wa Sudan Abdalla Hamdok amejibu kuwa fedha hizo zimeshatolewa tayari lakini hakukuwa na majibu ya haraka kutoka Marekani.
Sudan imekuwa katika orodha ya wafadhili wa ugaidi tangu mwaka 1993 wakati kiongozi wa al-Qaeda Osama Bin Laden alipoishi huko kama mgeni wa serikali.
Fidia hiyo inahusisha mabomu yaliolipuliwa na al-Qaeda mwaka 1998 katika balozi za Marekani barani Afrika.
Shambulio hilo lililotokea Tanzania na Kenya lilouwa watu zaidi ya 220 na fidia hiyo inapaswa kulipwa kwa wahanga na familia za waliopoteza ndugu zao”, bwana Trump alisema.
Uhusiano wa Marekani na Sudan umeimarika tangu rais Omar al-Bashir alipoweza kukabiliana na maandamano makubwa mwaka jana na hatimaye kuondolewa madarakani.