Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya mrisho kikwete April 17 2014 amepokea tuzo ya kiongozi bora wa maendeleo Afrika ambayo hutolewa na taasisi inayochapisha Gazeti la African Leadership la nchini Marekani.
Waziri wa Mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Benard Membe ambaye aliipokea tuzo hiyo nchini Marekani kwa niaba ya Rais Kikwete na kusema kutunukiwa kwa tuzo hiyo kulitokana na kushindanishwa katika vigezo mbalimbali.
Wasomaji wa gazeti hilo walimchagua Rais Kikwete kwa zaidi ya kura laki nne ambazo ndizo zilizomfanya kuwa mshindi kwa mwaka uliopita wa 2013 ambapo miongoni mwa sifa zilizomwezesha Rais Kikwete kutwaa tuzo hiyo ni pamoja na kuiendeleza nchi kiuchumi na kukuza maendeleo ya watu.
Baada ya President kuipokea alisema ‘tuzo ya Watanzania wote manake hayo mambo yanayosemekana yamefanyika chini ya uongozi wangu ni mambo ambayo tumeyafanya wote, mimi na viongozi wenzangu pamoja na Wananchi wa Tanzania ndio tumeweza kufanya haya ambayo leo yanaonekana duniani ni mema na kupewa tuzo’
Rais Kikwete amekuwa kiongozi wa tatu Afrika kupokea tuzo hiyo, ambapo kabla ya Rais Kikwete tuzo hiyo ilikwishatolewa kwa marais wa Sierra leone na Liberia.