November 3, 2020 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro Kamishna Msaidizi wa Polisi Emanuel Lukula amesema yoyote aliyepanga kuingia Mkoa wa Kilimanjaro kwa lengo la kuratibu maandamano asitarajie kutoka salama.
Aidha Lukula amewapongeza wakazi wa Mkoa wa Kilimanjaro kwa kutoitikia wito wa kufanya maandamano huku akiwataka kujikita katika uzalishaji bila ya kuwa na hofu yoyote.