Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi amemteua Hemed Suleiman Abdulla kuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee ilieleza kwamba Rais Dk. Mwinyi amemteua Abdulla kuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwa mujibu wa uwezo aliyopewa chini ya Kifungu Namba 39 (1) na 39 (2) cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.
Kabla ya Uteuzi huo Hemed Suleiman Abdulla alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba.Uteuzi huo umeanza jana Novemba 8, 2020
Katika utawala wa Rais Mstaafu Dk. Ali Mohamed She in nafasi hiyo ilishikwa na Balozi Seif Ali Idd ambapo amehudumu katika nafasi hiyo kwa miaka 10 mfululizo tangu mwaka 2010 hadi 2020.
Aidha Wengine walioteuliwa juzi Jumamosi ni Saada Mkuya Salum ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Fedha katika utawala wa awamu ya nne chini ya Rais Mstaafu Jakaya Kikwete.
Pia wengine walioteuliwa ni Tabia Maulid Mwita na Juma Ali Khatib.