Umoja wa Mataifa umesema Watu waliouawa nchini Nigeria katika shambulio la Boko Haram kwenye mashamba ya Mpunga ya Maiduguri ni 110.
Taarifa hii inapingana na ile iliyotolewa na Mamlaka za Nigeria ambapo walitaja watu 43 waliuawa katika shambulio hilo ambalo Raia walifungwa kamba kukatwa koo zao.
Ripoti zinasema Wakulima walishambuliwa na Boko Haram kwa kuwa walikuwa wanapeleka taarifa kwa Jeshi na kuwafichua walipo.
Mwezi uliopita Boko Haram iliwaua Wakulima 22 kwenye mashamba ya umwagiliaji katika matukio mawili tofauti. Serikali ilitangaza kuyashinda nguvu makundi hayo lakini imeonekana kuwa tofauti.