Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Dk. Tulia Ackson amesema ushirikiano ulipo kati ya Bunge na Serikali ni wa muhimu na siyo udhaifu kama inavyofikiriwa na baadhi ya watu.
Dk. Tulia ameyasema hayo Jijini Dodoma kwenye hafla ya uapishwaji wa wabunge Dk. Dorothy Gwajima na Mhandisi Leonard Chamlilo.
“Kwa mkutadha huo, tunamshukuru Rais Dk. John Magufuli kwamba Serikali iko tayari kusikiliza yale ambayo bunge inalishauri, isingekuwa hivyo hata haya tunayoyazungumza ingekuwa ngumu, sheria bunge ingeweza kutunga lakini serikali isichukue hatua yoyote” Dk. Tulia
“Lakini kutokana na kuchukuliwa kwa hatua mbalimbali na njema ndiyo maana wabunge sasa wako karibu zaidi na mawaziri n ahata hawa wanoenda kuapa kesho ni wazi kuwa ni mchango wako” Dk. Tulia
“Mfano hawa wabunge wasingeweza kupata fursa ya kuapishwa kesho kuwa mawaziri napengine isingetokea hiyo fursa labda mpaka bunge lijalo, lakini ni wewe uliyeleta hiyo hoja kwamba kuna wakati tunaichelewesha serikali sababu ya kanuni zetu” Dk. Tulia
“Lakini wewe uliliona hilo na ukafanya mabadiliko hivyo ni wazi kuwa hili ni moja ya mambo ambayo umefanya mabadiliko makubwa na chanya ambayo yataingia kwenye historia ya nchi hii, hata kama yatakuwepo maeneo ya hapa na pale lakini kazi unayoifanya Spika ni nzuri na kubwa” Dk. Tulia