Mwanza ni Miongoni mwa mikoa ambayo ukifika hata kama ukiwa mgeni huwezi kosa cha kufanya au ku-enjoy mbali na mji huu kuwa na vionjo vyake pia umejengwa kinamna yake ambayo kama hujawahi fika inaweza kukuacha hoi,hii ni baadhi ya nyumba kujengwa juu ya mawe tena milimani.
April 20 2014 rasmi Jembe ni Jembe Beach Resort imefunguliwa ili kutoa fursa kwa wakazi wa Jiji la Mwaza kufurahia mandhari ya beach hii ambayo iko pembeni kabisa ya Ziwa Victoria hapa pia zipo Boat ambazo zipo kwa wewe mwenye uhitaji kutembezwa ndani ya ziwa Victoria.
Skylight Band ndiyo bendi iliyotoa burudani kwenye usiku huu wa Pasaka ulioambatana na uzinduzi wa kiwanja hiki kipya,hizi ni baadhi ya picha za jinsi ilivyokua ndani ya Jembe ni Jembe Beach Resort.