Kurasa za mitandao ya kijamii ‘Facebook’ na Twitter za rais wa Marekani, Donald Trump zimeachiwa, baada ya kufungiwa kufuatia kuweka machapisho matatu yaliyokiuka maadili ya mitandao hiyo.
Katika mchapisho hayo, Trump alionyesha kuunga mkono vurugu zilizofanywa na wafuasi wake kwa kuvamia bunge la ‘Congress’ zilizosababisha vifo vya watu wanne na zaidi ya 50 kujeruhiwa.