Mbunge wa Jimbo la Mlimba mkoani Morogoro, Godwin Kunambi, amefanya ziara ya kikazi jimboni kwake ambapo amefanikisha upatikanaji wa ujenzi wa Daraja la Mto Mfuji katika kata ya Masagati ambao utagharimu Shilingi Milioni 53 na unatarajiwa kuanza Januari 13 mwaka huu huku pia akichangia Shilingi Milioni Saba kwenye Afya na Elimu.
Akizungumza katika ziara yake ya kuwatembelea wananchi hao Kunambi amesema yeye aliomba ridhaa ya kuwatumikia wananchi wa Mlimba hivyo ni jukumu lake kuhakikisha wanakua na miundombinu bora ya barabara, elimu na afya.
Kuhusu Maji Kunambi amesema tayari ameshapata kiasi cha Sh Milioni 50 ambacho muda wowote kitaingizwa kwenye akaunti ili kikatumike kuleta maji tiririka lakini pia kuchimba visima kwenye maeneo ambayo maji tiririka hayawezi kufika.
” Sitaki kuwa Mbunge wa kufanya mikutano, najua kero yenu ni hili Daraja hivyo fedha hizi tulizopata zitasaidia kuanza kwa ujenzi huu, lakini pia siyo kwenye ujenzi wa barabara pekee bali ninachangia maendeleo ya ujenzi wa sekta ya Afya na Elimu, kama ambavyo wananchi wengine wanachangishwa na mimi pia nitachangia, lengo ni kufanya Mlimba yetu ipae” Kunambi