Mahakama ya Tanzania itaanza kutoa muhtasari wa hukumu kwa lugha ya Kiswahili kuanzia Februari mwaka huu ikiwa ni sehemu ya mchakato wa kuanza kuendesha shughuli zote za Mahakama kwa lugha hiyo.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma, ameyasema hayo jijini DSM wakati akizungumzia maadhimisho ya Siku ya Sheria yanayotarajiwa kufanyika Februari Mosi, mwaka huu.
Maadhimisho hayo yatafanyika sambamba na Maadhimisho ya Miaka 100 ya Mahakama Kuu Tanzania.
Profesa Juma amesema, uendeshaji wa shughuli za Mahakama kwa lugha ya Kiswahili ni suala muhimu, lakini linahitaji umakini kulitekeleza.