Manispaa ya Milan nchini Italy imesema uvutaji sigara hautaruhusiwa katika maeneo ya wazi ikiwemo Bustani za Umma, Viwanja vya Michezo, Makaburi na Vituo vya Mabasi endapo kutakuwa watu wengine waliosimama eneo hilo.
Wavutaji sigara watakaovunja marufuku hiyo watatozwa faini ya fedha hadi Euro 240 (Takriban Tsh. 676,077). Milan ni moja ya Miji iliyo na uchafuzi mkubwa wa hewa Nchini Italia na Ulaya, na ulichukuwa uamuzi huu ili kulinda Afya ya Umma.
Pia, lengo la marufuku hiyo ni kupanua wigo wa marufuku ya kuvuta sigara katika miaka ijayo, na kupiga marufuku kikamilifu uvutaji sigara katika Mji huo ifikiapo mwaka 2025. Serikali imepanga kuweka marufuku ya fataki na uchomaji nyama nje ifikapo 2022.