Mkuu wa Wilaya ya Temeke Godwin Gondwe amemtaka Mkandarasi wa Kampuni ya SINOHYDRO inayotengeneza Barabara ya Mwendokasi awamu ya pili kuhakikisha anafanya kazi hiyo kwa thamani halisi ya fedha anayolipwa.
Kauli hii ya DC Gondwe imekuja baada ya kukagua na kugundua kasoro nyingi ikiwemo nyufa zilizoanza kwenye barabara hiyo na vituo vya mabasi ikiwa bado havijaanza kutumika.
“Siwezi kuona mradi mkubwa ambao Rais Magufuli anatoa pesa nyingi unahujumiwa halafu mimi nipo hapa,siwezi kukubali Temeke” Gondwe
“Kwa taarifa nilizonazo ninyi Viongozi wa hii kampuni ya SINOHYDRO mnawarubuni Vijana wetu waliopo maabara wakatae matokeo rasmi ya maabara na wakikataa mnawafukuza kazi”- Gondwe
Kwa upande wake Meneja mradi wa TANROADS, Injinia Barakael Mmari amemuhakikishia DC kuwa atahakikisha anafuatilia na kumwandikia kwa maandishi mkandarasi huyo.