Watu 38 wameuawa jana huko nchini Myanmar katika kile ambacho Umoja wa Mataifa umeelezea kuwa “siku ya umwagikaji mkubwa wa damu” tangu mapinduzi yalipofanyika mwezi mmoja uliopita.
Waandamanaji wamekuwa wakishinikiza kukomeshwa kwa utawala wa kijeshi na kuachiliwa huru kwa viongozi wa nchi hiyo waliochaguliwa – akiwemo Aung San Suu Kyi ambaye aling’olewa madarakani na kuzuiliwa wakati wa mapinduzi.
Uingereza imetoa wito wa kuitishwa kwa mkutano wa Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa, huku Marekani ikisema kuwa inatafakari kuwachukua hatua zaidi dhidi ya viongozi wa jeshi la Myanmar
Ghasia za hivi punde zinajiri siku moja baada ya majirani wa Myanmar kuomba majeshi kujizuia kufanya maafa zaidi.