Katika mwendelezo wakuadhimisha siku ya wanawake Duniani, kampuni ya Halotel Tanzania imeendelea kuunga mkono juhudi za wanawake wapambanaji katika majukumu yao ya kuleta mabadiliko chanya katika Nyanja mbalimbali ikiwemo kiuchumi, kijamii na kujenga taifa kiujumla.
Kutokana na ukweli kwamba wanawake wamekuwa wadau na mstari wa mbele katika kujikwamua kiuchumi, kifikra na kusaidia jamii, Kampuni ya simu ya Halotel imeendelea kutambua na kuthamini jitihada hizo kwa kutoa msaada wa hali na mali ikiwa ni moja ya ishara ya kuunga mkono juhudi hizo.
Katika muendelezo wa kuadhimisha siku hiyo ya wanawake Duniani, Halotel imetoa kiasi cha shilingi Milioni Tano (5,000,000/=) kwa kituo kinachoongozwa na mwanamke, ambacho kinalea watoto wenye ulemavu wa mfumo wa ufahamu kiitwacho Salt Vocational Training Center kilichopo eneo la Makabe Manispaa a Ubungo jijini Dra es saalam.
Kituo hicho ambacho licha tu ya kuwalea watoto hao kimekuwa kikitoa elimu ya ujuzi na ufundi stadi kwa watoto licha ya changamoto za ufahamu wanazokabiliana nazo.
Kiongozi wa kituo cha Salt Rebeka Lebi, amesema ‘’Kituo hiki kina watoto zaidi ya ishirini na mbili (22) ambao wanakabiliwa na changamoto za mfumo wa fahamu ikiwemo usonji, Udumavu, mtindio wa Ubongo na kifafa. Ambapo kutokana na changamoto hizi na wazazi ukosa kipato cha kuwasaidia, inapelekea kushindwa kupata masaada wa malezi ya karibu’’
Akielezea katika tukio la kukabidhi msaada huo, Afisa wa Habari Halotel Hindu Kanyamala, amesema “Halotel tunajisikia furaha kuendelea kusherehekea siku ya wanawake Duniani na mwanamama Rebeka Lebi, kiongozi na Mmiliki wa kituo cha Salt Vocational Training Center ,kwa kutambua na kuunga mkono juhudi zake kubwa za kulea watoto hawa tunatoa kiasi cha shilling Milion Tano za Kitanzania (5,000,000/-). Pia Tunampongeza kwa kuona umuhimu wa kulea na kutoa ujuzi kwa watoto hawa na kuleta mtazamo na matokeao chanya kwa jamii kwa ujumla. Hivyo kiasi hiki tulichokitoa tunaimani kitasaidia watoto hawa kusogea mbele Zaidi”
Kwa upande wake Kiongozi wa Kituo hicho Rebeka Lebi amesema, ‘’Tunashukuru sana uongozi wa kampuni ya Halotel kwa kutambua umuhimu wa kituo hiki na kile tunachokifanya, msaada huu umekuj kwa muda muafaka na utatusaidia katika ununuzi wa vifaa vya kufundishia na mahitaji mengine, hapa kituoni.
“Watoto hawa wamekuwa wakikumbwa na changamoto mbalimbali za kimalezi wanapokuwa majumbani, wengine wamekuwa wakipitia changamoto za unyanyasaji wa kijinsia na kutopata malezi bora, hivyo tukaona kupitia sisi Salt Center tunaweza badilisha maisha ya watoto hawa kwa kuwapa ujuzi ili waweze kuwa chachu na waweze kujitegemea na kushiriki katika ujenzi wa Taifa” Rebeka Lebi
Halotel itaendelea kushirikiana na jamii kwa kuisaidia kuleta maendeleo mbalimbali ikiwa ni njia mojawapo ya kurudisha shukuruani kwa wateja wetu na kuimarisha uchumi wa taifa letu. Sisi kama watoa huduma za mawasiliano maendeleo ya jamii ni maendeleo yetu pia kwasababu sisi sote tunatokea kwenye jamii.