Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) imesema ina deni kubwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan hususani katika usimamiaji wa kulipa Kodi.
Hayo yamebainishwa jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Taasisi hiyo, Angelina Ngalula ambapo amesema sekta hiyo inaunga mkono maagizo ya Rais Samia Suluhu Hassan na watashirikiana na Serikali katika hatua zote za utekelezaji wake.