Kuelekea sikukuu ya wafanyakazi duniani Mei Mosi 2021 rais washirikisho la vyama cha wafanyakazi Tanzania TUCTA Tumaini Nyamhokya amesema miongoni mwa mambo wanayoyatarajia wafanyakazi katika serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan ni nyongeza ya mishahara.
Nyamhokya ametoa kauli hiyo akiwa mkoani Tabora alipofika kukagua ujenzi wa ofisi ya chama cha wafanyakazi wa Serikali za Mitaa TALGWU mkoa zinazojengwa kupitia makusanyo kutoka kwa wanachama.