New Mexico imekuwa Jimbo jipya kuhalalisha matumizi ya Bangi kwa Watu wenye umri wa miaka 21 na zaidi baada ya Gavana Michelle Lujan Grisham kutia saini Miswada miwili kuwa Sheria.
Gavana Lujan Grisham amesema Sheria hiyo ni hatua kubwa kwa Jimbo lake. Bangi inayotumiwa kisheria itabadilisha Mitazamo na kuifanya New Mexico kuwa bora katika Nguvukazi, Uchumi na maisha ya baadaye.
Mauzo ya biashara ya Bangi yatazinduliwa kabla ya Aprili 1, 2022. Ushuru ambao utawekwa kwanza utakuwa 12% na mwishowe kwenda hadi 18% ili kukusanya mapato mengi kwa Serikali.
New Mexico sasa ni Jimbo la 17 kuhalalisha Bangi. Virginia ilipitisha mauzo ya Bangi mnamo Februari, lakini mpango wa kibiashara hautazinduliwa hadi 2024.