Mwanafunzi wa kidato cha nne Shule ya Sekondari Kabugalo, Gisera Oswardi (18) amefariki kwa kupigwa na radi huku mwalimu wa shule hiyo, Charles Alphonce akijeruhiwa.
Akizungumza Alphonce “Wakati natoka darasani naelekea ofisini nikiwa nimejifunika mwamvuli nimeongozana na Gisera nilisikia moto nikaanguka chini na kuanzia kiunoni kushuka miguuni nilikuwa kama nimepigwa ganzi, muda si mrefu walifika walimu kutupeleka hospitali,”.
Mganga Mkuu Mfawidhi Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Kagera, Mselata Nyakiroto amethibitisha kutokea kwa tukio hilo akibainisha kuwa alipokea taarifa ya majeruhi mmoja na maiti moja waliopigwa na radi.
“Hadi wanafika hospitali mwanafunzi alikuwa ameshafariki na mwalimu alikuwa na majeraha miguuni na kwenye mikono, amepatiwa matibabu anaendelea vizuri.” Mselata
“Uchunguzi wa awali umeonyesha kifo cha mwanafunzi kimetokana na radi kumuunguza sehemu kubwa za mwili wake,” Mselata