Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imeendelea kutoa tahadhari juu ya matarajio ya uwepo wa kimbunga Jobo kilichopo Bahari ya Hindi.
Kwa mujibu wa taarifa ya TMA iliyotolewa leo jijini DSM ni kwamba kimbunga hicho kinaendelea kusogea kuelekea maeneo ya Pwani ya Tanzania ambapo usiku wa kuamkia Aprili 24, 2021 (Jumamosi) kinatarajiwa kuwa umbali wa Kilometers 235 Mashariki mwa kisiwa cha Mafia.
Pia inaelezwa kuwa Jumamosi mchana ya Aprili 24, kitakuwa umbali wa Kilometers 125 Mashariki mwa Mafia.
Pia usiku wa kuamkia Aprili 25, kinatarajiwa kuendelea kupungua nguvu na kuwa mgandamizo mdogo wa hewa kikiwa katika mwambao wa Pwani ya Tanzania.
Vipindi vya Upepo mkali unaofikia Kilometers 50 hadi 60 kwa saa, mawimbi makubwa baharini pamoja na ongezeko la mvua kwa maeneo ya ukanda wa Pwani vinatarajiwa kujitokeza.
Maeneo yanayotarajiwa kupata athari za moja kwa moja kutokana na kimbunga Jobo Kisiwa cha Mafia, Lindi, Dar es Salaam pamoja na Unguja.