Siku chache baada ya video kusambaa ikimuonesha Mbunge wa Mtama Nape Nnauye akichangia moja ya mjadala uliohusisha Wabunge 19 wa Viti Maalumu akiwaita (COVID 19) akidai kuwa wamefukuzwa na Chama na jambo hilo liheshimwa na kwa kuwa Katiba iko wazi kwamba hakutakiwi kuwa na watu wasio na chama ndani ya Bunge.
Spika wa Bunge, Job Ndugai amesimama Bungeni leo na kumuonya Mbunge Nape Nnauye na wabunge wengine kuwa makini na maneno wanayoyazungumza.
“Juzi mdogo wangu Nape yalimtoka maneno na yamezunguka sana kwa sababu ni mbunge, ikifika mahali mbunge na Spika mnapishana nadhani haipendezi, kwa hiyo sitapitia hoja zake kwa sababu ana uhuru lakini kitu kimoja hana uhuru kwa sababu ya kanuni ni kuwasema vibaya wabunge wenzake kanuni zinakataza hilo lazima nilikemee, aliwataja kwa majina ya mitaani huko ambayo kwa kweli alikosea sana na niliongea naye naamini aliteleza kwa hiyo sitamsimamisha hapa aseme chochote ninachoombeni waheshimiwa mmsamehe bure aliwakosea sana, tuchunge sana midomo yetu tunapodeal na binadamu wenzetu”-Spika Job Ndugai