Waziri wa Viwanda na Biashara Prof.Kitila Mkumbo amesema mpaka sasa upatikanaji wa mafuta ya kula ni mkubwa hivyo hakuna haja ya kupandisha bei kwani mafuta yaliyopo yanajitoshereza kwa kipindi hiki na yanaweza kutumika hadi Mei 18 mwaka huu.
Akizungumza mapema leo Jijini Dar es salaam, mara baada ya kutembelea shirika la viwango Tanzania (TBS), Prof.Mkumbo amesema mpaka kufikia Tarehe 18 mwezi Mei, Meli zingine za mafuta zitakuwa zimeshawasili nchini hivyo hakutakuwa na adha yeyote ya upungufu wa mafuta.
“Hakuna sababu ya msingi kwa wafanyabiashara kupandisha bei ya mafuta kwasababu bidhaa ya mafuta ya kula ipo katika soko letu, hivyo bidhaa ipo ya kutosha na tutadili na wafanyabiashara wanaopandisha bei hovyohovyo” Prof.Mkumbo.
Pamoja na hayo Prof.Mkumbo amewapongeza TBS kwa juhudi wanazozifanya kuhakikisha bidhaa zote zinazoingia kutoka nje na ambazo zinazalishwa hapa nchini zinakuwa na ubora ambao unakubalika.
“Mpaka sasa hatuna rekodi ya bidhaa ambazo hazifai kwa matumizi ya binadamu. Hiyo inamaanisha kuna mtu anafanya kazi ya kudhibiti bidhaa ambazo hazifai na mtu huyo anaitwa TBS”. Prof.Mkumbo.
Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Shirika la Viwango Tanzania (TBS) leo Jijini Dar es Salaam mara baada ya kutembelea Shirika hilo.
Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Shirika la Viwango Tanzania (TBS) leo Jijini Dar es Salaam.Kulia kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Dkt.Athuman Ngenya.