Jeshi la wananchi Tanzania (JWTZ) Kanda ya Magharibi limewataka wananchi wa Mkoa wa Kigoma kushirikina na Vyombo vya Dola katika kulinda amani dhidi ya matukio ya Uhalifu mkoani Humo.
Hayo yameelezwa katika ufungaji wa zoezi la kijeshi la Excise Masika ambalo limefanyika kwa muda wa wiki moja katika pori la Makele Wilaya Kasulu Mkoani Kigoma.
Mwezi August 2019 Jeshi la Wananchi Kanda ya Magharibi lilifanya zoezi hilo ambalo lilitambulika kwa jina la KIKAKA katika eneo hilo ambalo linaelezwa kuwa changamoto ya uhalifu wa kutumia silaha na sasa hali inazidi kuimarika katika maeneo hayo.
Kanali Labani Thomas Mkuu wa Kikosi cha Jeshi 24 mkoani Kigoma amesema Wananchi wanatakiwa kuwa mstari mbele katika kuhakikisha vyombo vya dola vinafanya kazi yake vyema katika kulinda amani.