Mkurugenzi wa mawasiliano ya rais Ikulu, Gerson Msigwa amewataka Watanzania kupuuza taarifa zilizorushwa na televisheni moja ya nchini Kenya kwamba Rais wa Tanzania, Samia Suluhu ameagiza wafungwa kwa kisiasa nchini kuachiwa huru.
“Kuna jambo tumeona tulitolee ufafanuzi Kuna clip inazunguka ikisema Rais Samia Suluhu ametoa agizo la kuachiwa huru kwa Wafungwa wa Kisiasa 23, sio kweli Rais hajazungumza suala hilo, pili Nchi yetu haina Wafungwa wa Kisiasa, Watanzania wapuuze taarifa hizo” Gerson Msigwa, Msemaji Mkuu wa Serikali akiwa Dar es salaam leo
“Hiki Chombo cha Habari cha Nchi jirani nisingependa kukitaja tunaamini wataomba radhi na kufuta taarifa hiyo, tayari Ofisi yetu ya Ubalozi Nairobi inafuatilia kujua kwanini wamepotosha” Msigwa