Kuelekea Siku ya Vipimo Duniani Mei 20,Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limewataka watumiaji wa Vipimo katika sekta ya afya nchini kuhakikisha vipimo hivyo vimepitishwa na Shirika hilo kabla havijatumika.
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam Afisa Vipimo Mwandamizi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Bw.Ramadhan Mkumba amesema wamekuwa wakikutana na Changamoto kubwa ya watumiaji wa Vipimo kutokuwa na uwelewa wa kufanya uhakiki wa vifaa vyao ili kuboresha huduma wanazozitoa kwenye sekta za afya.
“Vipimo vinavyotumika katika sekta ya afya ni muhimu vikahakikiwa na kujulikana ubora wao kwa kufanya hivi itakuwa inalinda afya ya wagonjwa kwasababu daktari anaweza kufanya maamuzi kupitia vipimo vinavyotoka maabara vikiwa vipimo sio sahihi vinaweza kupelekea kumpatia madhara mgonjwa”.Mfaume.
Aidha Bw.Mfaume amesema kuwa dhumuni la kauli mbiu ya mwaka huu ni kuleta uelewa katika jamii jinsi gani vipimo kwenye sekta ya afya vina umuhimu kama tunavyotambua vipimo katika sekta ya afya vinatumika kugundua, kutambua na kutibu magonjwa.
Kwa upande wake Mkuu wa Maabara ya vipimo (TBS), Bw.Joseph Mahila amesema katika maadhimisho ya Siku ya Vipimo kwa mwaka huu watajikita zaidi katika sekta ya afya hasa kutokana na kauli mbiu ya mwaka huu “VIPIMO KATIKA SEKTA YA AFYA”.