Halmashauri ya Manispaa ya Temeke ambayo ina ukubwa wa Kilometa za mraba 656 ambayo ina jumla ya watu 1,368,881 ambayo ni kwa mujibu wa taarifa ya sensa ya mwaka 2012 ambayo hii inamaanisha tarafa 3 ambazo ni Mbagala,Chang’ombe na Kigambonina kujumuisha kata 30 na mitaa 180 na maafisa afya 75 wanaohudumia manispaa hii.
Mpaka sasa hatua ambazo manispaa ya Temeke imechukua ili kusimamia usafi wa Manispaa ni pamoja na kuweka sawa sehemu ambazo zilikua zinaonyesha kutokua sawa ambapo jumla ya meza 2193 zimevunjwa,idadi ya mabanda yaliyovunjwa ni 415,jumla ya watuhumiwa 172 walikamatwa na watu 92 walipewa onyo kali.
Waliotozwa faini za papo hapo ni 80 ambapo ilipatikana Tsh.4,120,000 mpaka sasa watu 45 wamepelekwa mahakamani na kesi zao zinaendelea na jumla ya Ombaomba 74 walikamatwa na kurudishwa makwao.