Leo rasmi zimezinduliwa tuzo za Chaguo la Mteja ambalo Kwa sasa limefungua dirisha la washiriki katika mataifa mengine ndani ya Bara la Afrika na uzinduzi huu ume zinduliwa rasmi na mgeni rasmi ambaye alikuawa Balozi mteule na Mkurugenzi Mkuu wa TANTRADE Edwin N Rutageruka.
Katika uzinduzi huu pia imetangazwa rasmi ubia ambao Consumer Award imeingia na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara ambapo Taaasisi ya Maendeleo ya Biashara (TANTRADE TANZANIA) ndio wasimamizi rasmi wa maandalizi wa tuzo hizi na kuahidi kutupa ushirikiano kwanzia sasa mpaka hatua ya mwisho.
Pamoja na TanTrade, Consumer Award imetangaza rasmi watakao wasimamia zoezi zima la upigaji kura na kuhakiki matokeo, ambao ni PWC Tanzania, hii ni katika kuhakikisha matokeo ya Tuzo yana kuwa yenye kuaminika-
Tuzo za Consumer Choice Awards kwa mwaka huu wa 2021 zinatarajiwa kupiga hatua zaidi ya pale zilipokomea mwaka jana 2021.
Tuzo hizo za chaguo la walaji ambazo kwa miaka ya nyuma zilikuwa zikifanyika ndani ya Tanzania tu kwa sasa zitaenda kwenye nchi nyingine barani Afrika kwa kuhusisha makampuni na watu mbalimbali ambapo sasa zitafahamika kama Consumer Choice Awards Africa.