Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Amos Makalla leo ametangaza Vita na Mtandao wa wezi wa mafuta ghafi kupitia bomba kuu la mafuta *Kigamboni na kulielekeza Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam kuwashughulikia wahalifu wa mtandao huo.
RC Makalla ameyasema hayo wakati wa ziara ya kukagua miundombinu ya Kupokea Mafuta ghafi kutoka kwenye Meli za Mafuta hadi kwenye Visima ambapo ameshuhudia uharibifu mkubwa wa miundombinu uliofanywa na Mkazi mmoja aliechimba handaki hadi kwenye Bomba kuu la mafuta na kujiunganishia.
Kutokana na Wizi huo RC Makalla ameeleza kutoridhishwa na maelezo aliyopewa na TPA na Wakala wa uagizaji Mafuta kwa pamoja na kuamua kuhitisha kikao cha pamoja Siku ya Jumatatu kwenye ukumbi wa Anatoglo kitakachojumuisha Waagizaji Mafuta, TPA, TRA na Wadau wote wa Mafuta ili wajadili namna bora ya kuhakikisha *tatizo hilo halijirudii na kupitia mikataba yao hususani kipengele cha namna gani mfanyabiashara aliepokea Mafuta pungufu tofauti na Yale aliyolipia anafidiwa.