Uharibifu mkubwa uliofanywa na panya mmoja katika eneo la New South Wales, Australia, umelazimisha gereza moja kuwahamisha mamia ya wafungwa ili kufanya ukarabati na usafi.
Zaidi ya wafungwa 400 na wafanyakazi 200 wa gereza laWellington watahamishiwa kwenye magereza mengine katika kipindi cha wiki mbili zijazo.
Panya huyo amesababisha uharibifu mkubwa kwa miundo mbinu ya gereza, ikiwa ni pamoja na nyaya za ndani ya gereza pamoja na paa.
Mavumo yameongeza hivyo idadi ya panya katika jimbo hilo lililopo Kusini-Mashariki mwa Australia, ambako wanyama hao wamekuwa wakifanya uharibifu mkubwa wa mazao mashambani.
Maafisa wa magereza ya taifa hilo wanasema wafungwa katika gereza hilo watapunguzwa kwa miezi minne huku likisafishwa, kukarabariwa na kulindwa dhidi ya uharibifu siku za usoni.