Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Jokate Mwegelo ameeleza dhamira yake ya kubadilisha taswira ya muonekano wa eneo la mbele ya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ambalo linatazamana na Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kwa kuweka taa za kisasa 32.
Akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya kukutana na Maafisa wa TARURA, Jokate amesema eneo la ofisi ya Mkuu wa Wilaya linatazamana na Uwanja wa Benjamin Mkapa ambalo hukutanisha Maelfu ya Watanzania na Watu wa Mataifa mbalimbali, hivyo ni vizuri taswira yake ikaendana na hadhi hiyo.
Amesema ana taarifa za uhalifu nyakati za usiku ambapo eneo hilo kwa kukosa taa huwa na kiza kinene, kinachopelekea wepesi wa vitendo viovu kufanyika———“Mimi ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Wilaya ya Temeke haitaleta afya hata kidogo uhalifu kufanyika eneo la Ofisi ya DC ”
Meneja wa TARURA ambaye pia ni mratibu wa uendelezaji Jiji la Dar es Salaam, amesema kuwa zoezi la ukarabati na uwekaji wa taa 32 katika eneo hilo la Barabara lenye urefu wa kilometa 1.3 litagharimu kiasi cha zaidi ya Tsh. milioni 102 na litakamilika baada ya Wiki mbili.