Filamu ya Binti inapeperusha bendera ya Tanzania kimataifa kwa kuchaguliwa kuingia kwenye Tamasha la Durban Film Festival nchini Afrika Kusini.
Ni filamu ya kwanza ya Tanzania kuwahi kuchaguliwa kuoneshwa kwenye tamasha hilo toka tamasha ilipoanzishwa mwaka 1979.Durban imechagua filamu 100 tu kati ya 3,000 duniani kucheza kwenye tamasha hilo mwaka huu. Na maonyesho yatanfanyika 22 Julai mpaka tarehe 1 Agosti mwaka huu.
Filamu hii pia imeongozwa na mrembo Seko Shamte ambae aliwahi kusimamia filamu zilizowahi kufanya vizuri ikiwemo Homecoming pamoja na Mkwawa.
Filamu inamshirikisha Gordian pamoja na Maggie Vampire kama wachezaji na ndani yake inatumia nyimbo za wasanii wa hapa hapa nyumbani kama Young lunya pamoja na Turu nesh.
Seko anasema “tunaendelea kujitahidi kuwasilisha filamu zetu kimataifa ili tutangaze vipaji ya vijana wa hapa nchini. Nimefurahi sana na tunawashukuru Durban Film Festival kwa kutupa hii heshima kubwa sana’- Seko Shamte
UNAWEZA UKABONYEZA PLAY KUITAZAMA TRAILER YA BINTI HAPA
KAMA ULIMISS UZINDUZI WA FILAMU YA BINTI BASI UNAWEZA UKABONYEZA PLAY KUITAZAMA HAPA