Wakati Jeshi la polisi likimshikilia Askari wa Jeshi la Wananchi kwa tuhuma za mauaji ya Lais Lemomo mkazi wa kijiji cha Lashaine Wilayani Monduli Mkoani Arusha, Familia ya Kijana huyo imelaani kitendo kilichofanywa na Askari huyo huku wakiomba Serikali kuingilia kati suala hilo kwa kuwa Kijana huyo alikuwa akichunga mifugo kwenye eneo la Wananchi.
Kaka wa Marehemu Melubo Laizer ameomba kilio chao kufika kwa Viongozi wa juu kwa kuwa kitendo hicho ni cha uonevu kutokana na kuuawa kwa Mdogo wake.
Mkuu wa Wilaya ya Monduli Frank Mwaisumbe amekiri kutokea kwa tukio hilo na alifika eneo la tukio baada ya kupata taarifa kutoka kwa Wananchi na suala hilo lipo Polisi.