Waziri wa Maji, Jumaa Aweso ameagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru)) kuchunguza utekelezaji wa ujenzi wa mradi wa bwawa la kuhifadhia maji la Maratani Wilayani Nanyumbu, Mtwara ambalo limegharimu kiasi cha Sh1.139 bilioni.
Lengo la wito huo ni kubaini thamani ya fedha iliyotumika na hali halisi iliyoonekana katika mradi ambayo hairidhishi.
Waziri Aweso katika ukaguzi huo amekuta umati wa wananchi wakimsubiri na kulalamika kuhusu changamoto kubwa ya maji safi inayowakabili.
Utekelezaji wa Ujenzi wa bwawa hilo umefanywa na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA)kupitia Idara ya Uchimbaji-DDCA.