Polisi Dar es salaam wanawashikilia Watu wanne kwa tuhuma za kutishia Watu kwa bastola wanazozimiliki kihalali ambapo Watuhumiwa wote silaha zao zinashikiliwa na Polisi na taratibu za kisheria zitafuatwa ikiwa ni pamoja na kuwafutia umiliki wa silaha hizo.
Kamanda Muliro amesema “Watuhumiwa hao ni Isack Robert Wile maarufu Wambura,(44), Mkazi wa Sinza E, Rashid Iddi Mshana (36), Mkazi wa Mwenge, Mussa Rashid Mshana,(39), Mkazi wa Mwenge na Ibrahim Shaibu,(52),Mkazi wa Kinyerezi”- Polisi
“Mtuhumiwa wa kwanza, Isack Robert Wile (Wambura) akiwa katika Bar iliyopo Sinza alitoa silaha yake bastola aina ya Browning yenye namba TZCAR 72791 na kuanza kutishia Watu huku akiwa amelewa pombe”-asema Kamanda Muliro.
“Mtuhumiwa wa pili, Rashid Iddi Mshana alionekana kwenye video clip iliyosambaa kwenye mitandao akitishia, Polisi walimkamata Mtuhumiwa huyo akiwa na silaha bastola yenye risasi 10 ndani ya magazine ikiwa inamilikiwa na kaka yake aitwae Mussa Rashid Mshana”- asema Kamanda Muliro.
“Mtuhumiwa wa tatu Mussa Rashid Mshana anatuhumiwa kwa kosa la uzembe ambapo alimwachia silaha mdogo wake ambaye ni Rashid Iddi Mshana ambae alijirekodi akitishia Watu kwa silaha na kutuma clip kwenye mitandao ya kijamii”- asema Kamanda Muliro.
“Mtuhumiwa wa nne, Ibrahim Shaibu Aug 1 saa 12:00 jioni maeneo ya Vijibweni Kigamboni alimtishia kumuua kwa silaha jirani yake aitwae Chacha Mwita walipokuwa wanagombania mipaka ya kiwanja katika maeneo yao, Mtuhumiwa alikamatwa akiwa na silaha bastola aina ya LUGER ikiwa na risasi 06”-asema Kamanda Muliro.
MADEREVA 6 WA BODABODA KUFIKISHWA MAHAKAMANI “PIKIPIKI HAZINA LESENI/KUPAKIA ABIRIA ZAIDI YA MMOJA”