Ni Agosti 12, 2021 ambapo huduma ya utoaji chanjo ya kujikinga na Corona imeendelea kwa wakazi wa Dar ambapo Watu mbalimbali wakiwemo Wasanii, Waandishi wa Habari na wengineo walifika kujipatia huduma hiyo.
Akizungumza Katibu Mkuu Wizara ya Afya Prof. Abel Makubi alisema chanjo hiyo kwa sasa itatolewa kwa wote kuanzia na wenye umri wa miaka 18 na kuendelea, huku wazee wakiendelea kuwa kipaumbele wakati wanapofika katika vituo hivyo.
“Hapo tuko kwenye zoezi la kuchanja katika kituo cha Karimjee na mpaka sasa tumechanja watu 150 na Wananchi wa makundi yote na lengo ni kuwapa huduma Wananchi ambapo wanahitaji huduma hii ili wasisumbeke kwenda Mahospitali kwahiyo Watu ambao wapo katika maeneo ya Posta basi apite hapa muitikio ni mzuri na kuchanja ni hiari”- Katibu Mkuu Wizara ya Afya Prof. Abel Makubi
WASANII, WANAMICHEZO NA WANAHABARI CHANJO KARIMJEE, MAKATIBU WAZUNGUMZA