Akizungumza na Wahariri wa Vyombo vya Habari nchini Kenya, Rais Kenyatta amesema anashangazwa na mwenendo wa naibu wake ambaye anapinga mipango ya serikali ambayo anaitumikia.
Rais Kenyatta amesema hakuwa na shida na Ruto kujenga ngome yake kisiasa lakini alihoji njia ambazo zinatumika katika chama kipya cha Ruto kiitwacho UDA.
“Mimi niko na ajenda ambayo nilichaguliwa kwa ajili yake na kazi hiyo lazima iendelee na itafaa sana jambo la busara kufanya kama hufurahishwi nayo basi unafaa kusonga kando”– Rais Kenyatta
“Na kuruhusu wanaotaka kuendelea waendelee halafu upeleke ajenda yako kwa Wananchi watu wanajua kinachotendeka mnapokosa kukubaliana katika demokrasia iliyo na maendeleo na ustaarabu basi natarajia watu wanaweza kuwa na ujasiri wa kufanya hivyo”– Rais Kenyatta
Uhuru aliongeza kuwa alishangaa kwanini naibu wake alikuwa akipinga mchakato wa BBI akisema… “Maswala yaliyopelekea kuundwa kwa BBI ndio yale yale yaliyowaleta pamoja”.
“Ninafurahia kumaliza muda wangu na kutekeleza mipango yangu lakini naamini pia hii ni mojawapo ya ajenda yangu kuweza kuwaleta Watu pamoja na kuweza kuhakikisha kuwa tuko na Nchi iliyo na Amani na Umoja”- Rais Kenyatta
“Na ndio maana nilifuatilia kwa karibu kwa bahati mbaya, koti imetoa uamuzi wake na ninaamini walipewa mawaidha mabaya katika mchakato huo, kwa bahati mbaya kumekuwepo na misimamo ya kupata faida kisiasa kwa muda mfupi ambazo hawaulizi tena kwanini tulitaka BBI na sasa wamelifanya swala la ushindani na sijui ni kwanini”- Rais Kenyatta
Ruto ameahidi kuunda serikali kwa kuwajumuisha watu wanyonge katika jamii ili kujenga uchumi na taifa dhabiti.
Source BBC Swahili
ASKOFU GWAJIMA BAADA YA KUHOJIWA, M/KITI ASEMA AMETUPA USHIRIKIANO