Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi maarufu (Mahakama ya Mafisadi), inatarajia kutoa uamuzi Septemba 1, 2021 kama ina mamlaka ya kusikiliza kesi ya Uhujumu Uchumi na Ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na wenzake ama lah.
Kesi hiyo imetajwa leo mbele ya Jaji Luvanda ambapo upande wa washitakiwa ukiwakilishwa na Wakili Peter Kibatala uliibua hoja ya kutaka kesi hiyo ifutwe kutokana na Mahakama ya Mafisadi kutokuwa na uwezo wa kusikiliza kesi za Ugaidi.
Hata hivyo, upande wa Jamhuri ulipinga hoja hiyo na kusema Mahakama hiyo ina mamlaka.