Ni Septemba 2, 2021 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwa njiani kuelekea Bagamoyo kwa ajili ya kuandaa documentary ya kuutangaza utalii.
Sasa msafara wake ukasimama katika Tegeta Dar es Salaam kisha akaongea na Wananchi.
“Kwenye bajeti iliyopita tuliweka tozo ya miamala, imepigiwa kelele sasa tumepunguza 30% ila tozo zitaendelea kuwepo sitaki kuwaficha kwa miezi hii miwili tu tumekusanya zaidi ya Bilioni 60 na zitawezesha kujenga vituo 220 vya afya” – Rais Samia
“January tuna wimbi kubwa la Watoto wanaoingia Sekondari na wale wanaojiunga Darasa la kwanza, pesa tutazozikusanya September na October,2021 tutajenga madarasa zaidi ya 500, kuna mambo mengi mfano la Shule kama hili aliloliomba Mbunge (Gwajima), niwahikikishie Shule itajengwa nitaiomba TAMISEMI kwenye hizo fedha za makusanyo ya tozo nyingine ziletwe Kawe zijenge Shule”- Rais Samia
“Binadamu ukifanya watasema usipofanya watasema bora tufanye wakione kuliko waseme wakati hatujafanya
Kelele za mlango hazimuachishi mwenye nyumba kulala kwasababu tumezizoea, kusemwa kupo tu”——— Rais Samia leo akiwa Tegeta kuelekea