Ni Septemba 10, 2021 ambapo wakati Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiahirisha Mkutano wa nne wa Bunge la 12 la JMT aligusia mchezo wa masumbwi (Ngumi).
Majaliwa alipongeza kitu cha Matangazo cha Azam kwa kuendelea kuupa kipaumbele mchezo huo.
Aidha akasema anatamani siku moja kushuhudia pambano la Twaha Kiduku dhidi ya Hassan Mwakinyo wazichape ulingoni.
“Nitumie nafasi hii pia kukipongeza kituo cha matangazo cha Azam (Azam Media) hususan upande wa matangazo ya runinga kwa kuibua na kuutangaza vyema mchezo wa masumbwi nchini, juhudi hizo za Azam Media wakishirikiana na wadau wengine zimewezesha wanamasumbwi wetu kutumia vizuri fursa hiyo kukuza vipaji vyao”
“Nimpongeze Twaha Kiduku kwa kumtwanga Dulla Mbabe katika pambano lililovuta hisia za Watanzania wengi, vilevile nimpongeze Bondia Hassan Mwakinyo kwa kumdunda mpinzani wake Mnamibia Julius Indongo kwa TKO na kutetea mkanda wake wa Chama cha Ngumi Afrika (ABU)”
“Wanamasumbwi wetu wameendelea kuifanya Tanzania itambulike zaidi ulimwenguni sasa tunasubiri pambano la watani Mwakinyo dhidi ya Kiduku” ——— Waziri Mkuu Majaliwa akiahirisha Mkutano wa nne wa Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
KWA WANAOSUBIRI PAMBANO LA HASSAN MWAKINYO NA TWAHA KIDUKU