Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi inatarajia kutoa uamuzi Oktoba 19, 2021 wa kesi ndogo ndani ya kesi ya msingi baada ya Upande wa Utetezi kufunga ushahidi katika kesi ya Uhujumu Uchumi na Ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na wenzake.
Kesi hiyo ndogo ndani ya kesi ya msingi inasikilizwa mbele ya Jaji Mustafa Siyani ambaye atatoa uamuzi Oktoba 19, baada ya leo shahidi wa Utetezi, Lilian Furaha Kibona ambaye ni mke wa mshitakiwa Adam Kasekwa kumaliza kutoa ushahidi.
Uamuzi huo mdogo unatokana na pingamizi ambalo liliwekwa na Upande wa utetezi kuhusiana na kielelezo cha Upande wa Mashitaka kinachodaiwa kuwa ni maelezo ya mshitakiwa Kasekwa.
Mbali na Mbowe na Kasekwa, washitakiwa wengine ni Halfan Bwire na Mohammed Ling’wenya.
SHAHIDI: KOMANDOO JWTZ ALIVYOIMBA WIMBO WA KIJESHI MAHAKAMANI, ULIKUWA UTEKAJI, BILA KULA SIKU 10